Habari

Imewekwa: 16/03/2021

TAARIFA KWA UMMA

TAARIFA KWA UMMA

Dar es Salaam- 16 Machi, 2021

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) inapenda kuwataarifu Wauzaji (Expoters) wa bidhaa za Kilimo, Mifugo na Uvuvi na bidhaa za Viwandani kwenda nje ya nchi kuwa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) inatoa udhamini wa mauzo ya bidhaa nje ya nchi (Export guarantee).

Udhamini huu unalenga kuwasaidia wafanyabiashara kuweza kupata mkopo wa kuweza kusafirisha na kuuza bidhaa zao nje ya nchi.

Ili kupata udhamini huu mfanyabiashara anatakiwa kukidhi vigezo vifuatavyo:-

1.Awe na biashara rasmi iliyo na leseni na vibali vya kufanya biashara nje ya nchi.

2.Awe na makubaliano (mkataba) na mnunuzi wa bidhaa husika nje ya nchi.

3.Awe na uzoefu wa kufanya biashara nje ya nchi kwa muda wa miaka miwili au zaidi

Endapo unakidhi vigezo/masharti tajwa hapo juu tafadhali Bofya hapa kupakua na ujaze dodoso hili kikamilifu na kuliwasilisha kwa barua pepe info@tantrade.go.tz . Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana nasi kwa simu namba 0735 647 165 au unaweza kutembelea ofisi zetu Kitengo cha Taarifa za Biashara zilizopo katika uwanja wa Maonesho wa Mwl. J.K.Nyerere barabara ya Kilwa.