Habari

Imewekwa: 08/11/2019

TAARIFA KWA UMMA

 TAARIFA KWA UMMA

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) inapenda kuwataarifa wazalishaji wa bidhaa mbalimbali, wafanyabiashara na umma kwa ujumla kuwa,

  • 1.Ili kupata taarifa za biashara na masoko ya ndani na nje ya nchi unaweza kupiga simu bure bila tozo yoyote kupitia namba 0800110134 na
  • 2.Kama unakutana na vikwazo, changamoto au kero za kibiashara hasa zile zisizokuwa za kikodi (NTBs) katika mipaka ya Tanzania unaweza kupiga simu bure bila tozo yoyote kupitia namba 0800110133

Endapo utaridhika au hutaridhika na huduma wasilisha malalamiko yako kwa barua pepe feedback@tantrade.go.tz. Huduma zote zitazingatia taratibu za muongozo wa mkataba wa huduma kwa mteja.