Habari

Imewekwa: 02/06/2019

USAJILI WA VITAMBULISHO KWA WASHIRIKI WA MAONESHO YA 43 YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA DAR ES SALAAM

USAJILI WA VITAMBULISHO KWA WASHIRIKI WA MAONESHO YA 43 YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA DAR ES SALAAM

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) inapenda kuwataarifu washiriki wote wa Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam kuwa Huduma ya Usajili wa Vitambulisho kwa njia ya Kielektroniki imefunguliwa rasmi kupitia https://ditf.tantrade.go.tz au tovuti www.tantrade.go.tz.

Mamlaka inawashauri waratibu wote watakaoshiriki Maonesho kujisajili kwa kuwasilisha taarifa za washiriki wao ili wapate vitambulisho mapema kabla ya kuanza Maonesho tarehe 28 Juni, 2019.

Aidha,TanTrade inawashukuru sana kwa kukubali kushiriki Maonesho haya muhimu yenye lengo la kuendeleza biashara na huduma kwa maendeleo ya viwanda hapa nchini.

Kwa taarifa/ufafanuzi zaidi tafadhali wasiliana nasi kupitia simu Na.0757 240199 (Bw Dagobert Kahanda) na barua pepe dagobert.kahanda@tantrade.go.tz au kwa namba ya simu Na.0717 508085 (Bw Hamisi Mikaro) barua pepe hamisi.mikaro@tantrade.go.tz