Habari

Imewekwa: 03/10/2020

TAARIFA KWA UMMA

TAARIFA KWA UMMA

KONGAMANO LA KIMTANDAO (WEBINAR) JUU YA UWEKEZAJI WA VIWANDA

LITAKALOHUSISHA MAKAMPUNI MADOGO, YA KATI NA MAKUBWA (SMEs) KATI

YA TANZANIA NA NCHI ZA NORDIC

Dar es Salaam - Tarehe 02 Oktoba, 2020

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) inapenda kuwataarifu

Wafanyabiashara, Wazalishaji wa Bidhaa za Kitanzania na Umma kwa ujumla kuwa, Alhamis

tarehe 8 Oktoba, 2020 kutakuwa na Mkutano wa Kielektroniki ulioandaliwa na Ubalozi wa

Tanzania nchini Uswidi kwa kushirikiana na Chama cha Biashara cha Norway - Afrika (NABA).

Lengo la mkutano huo ni kuhamasisha biashara baina ya Bara la Afrika na nchi za NORDIC

ambazo ni Uswidi, Norway, Ufini, Denmark na Iceland na unatarajiwa kukutanisha washiriki

wapatao 400 kutoka nchi 35 na makampuni 150 katika sekta za Nishati, Huduma za usafirishaji

majini (Shipping), Teknolojia, Bidhaa za Viwanda, Kilimo, na Uvuvi, Biashara ya majengo (Real

estate), na Utalii kutoka ukanda wa Nordic.

Kwa mujibu wa tathmini ya mahusiano ya kibiashara kati ya Tanzania na NORDIC mazao ya kilimo

yenye fursa kubwa ya biashara ni pamoja na Kahawa, Parachichi, Samaki na Kamba (Shrimps &

Prawns), Korosho, Maua, Ufuta, Chai, Mafuta ya Alizeti, Mashudu ya Alizeti na Nguo za Pamba.

Hivyo, Wafanyabiashara na Wazalishaji walio katika sekta husika wanahamasishwa kushiriki

mkutano huu muhimu, ili kufahamu namna ya kufikia fursa ambayo itawezesha biashara baina ya

Afrika na nchi za Nordic kufanyika.

Ili kujisajili tafadhali tembelea tovuti www.webcast.norwegianafrican.no/register Kwa taarifa zaidi

tafadhali wasiliana na Bw. Ruperto Mboya kwa simu Na. +255 713 380 748 au Barua pepe:

info@tantrade.go.tz

Imetolewa na:

Theresa H. Chilambo

Mkuu wa Kitengo cha Mawasilianowasiliano