Habari

Imewekwa: 14/03/2019

FURSA YA MASOKO YA MATUNDA NA VIUNGO

FURSA YA MASOKO YA MATUNDA NA VIUNGO

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania inapenda kuwataarifu kuwa imepokea maombi kutoka kampuni ya Kitanzania yenye uhitaji bidhaa ifuatayo kutoka kwa wazalishaji wa Kitanzania; 1. Mapapai yenye uwekundu kwa ndani (Red lady Variety), 2. Iliki ya Kijani (Green Cardamon) Tani mbili (2), 3. Majani ya mpapai tani saba (7) yenye rangi ya kijani kama picha inavyoonesha hapa chini; Ikiwa unakidhi vigezo tuma maombi yako kupitia barua pepe info@tantrade.go.tz. Kwa maelezo zaidi tafadhali tembelea ofisi zetu zilizopo kwenye Uwanja wa Maonesho wa Mwl J.K.Nyerere, Barabara ya Kilwa au kutupigia simu kupitia namba 0735 510907 (Bi Miriam Kikoti) Mwisho wa kutuma maombi haya ni tarehe 19 Machi, 2019

Imetolewa na;

Theresa H. Chilambo

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano

13 Machi, 2019