Habari

Imewekwa: 05/03/2019

FURSA YA MAFUNZO KWA WADAU WA PARACHICHI NA VIUNGO

FURSA YA MAFUNZO KWA WADAU WA PARACHICHI NA VIUNGO

Kituo cha Biashara ya Kimataifa (ITC) kwa kushirikiana na Taasisi inayosimamia Wadau wa Matunda, Mbogamboga na Viungo (TAHA) chini ya ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU) unatekeleza mradi wenye lengo la kuboresha masoko ili kuongeza mauzo ya nje ya nchi (MARKUP)

Tunapenda kuwataarifu Wazalishaji na Wafanyabiashara wa Kitanzania Wadogo na wa Kati (SMEs) wanaojishughulisha na mazao ya Parachichi na Viungo (Spices) kuwa, kutakuwa na mafunzo ya siku tatu (3) ya kuandaa mkakati wa kuuza bidhaa hizo nje ya nchi. Mafunzo hayo yatalenga katika Kusimamia Ushindani wa Biashara, Kuandaa Mkakati wa Kuuza Nje, Kufanya Miamala ya Kuuza Nje na Kuandaa Mpango wa Biashara wa Kuuza Nje ya nchi.

Hivyo, Vigezo vya Kushiriki Mafunzo hayo ni kama Ifuatavyo:

1.Kampuni Ndogo na za Kati zinazojishughulisha na uzalishaji au biashara ya Parachichi na Viungo (Spices);

2.Kampuni yenye uzoefu wa kuuza bidhaa hizo nje ya nchi au inatamani kuanza kuuza nje ya nchi;

3.Kampuni iwe na mifumo ya usimamizi na uendeshaji wa biashara;

4.Kampuni iwe tayari kuboresha mifumo ya uendeshaji biashara;

5.Utayari wa kutoa na kushirikisha taarifa za biashara na kutekeleza mapendekezo ya mikakati wa kuuza nje ya nchi yatakayotolewa;

6.Utayari wa kuandaa Mpango Biashara wa Kuuza nje ya nchi na kukamilisha majukumu utakayopangiwa ndani ya muda uliokubaliwa;

7.Kampuni iwe na mifumo pamoja teknolojia ya uzalishaji;

8.Kampuni iwe tayari inafanya biashara katika soko la ndani ya nchi na

9.Kampuni iwe na wanunuzi wengi katika soko la ndani na nje ya nchi au iwe tayari kutanua uwigo wa biashara na kuongeza wateja.

Ili kushiriki tafadhali pakua fomu hapa na kuwasilisha maombi yako kwa barua pepe ifuatayo leite@intracen.org nakala kwa adallo@intracen.org , eric.mwesigwa@taha.or.tz, na asha.malanga@tantrade.go.tz Kwa mawasiliano zaidi waweza kupiga simu kupitia namba 0787 654386 (kwa wadau wa Parachichi) na 0655 443871 (kwa wadau wa Viungo).

Mwisho wa kutuma maombi ni Machi 8, 2019.