Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TanTrade Yafanya Mkutano na Wanachama wa CTI Kuhamasisha Matumizi ya Nembo ya Taifa – Made in Tanzania

  • February 25, 2026


Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imefanya mkutano na wanachama wa Chama cha Wamiliki wa Viwanda Tanzania(CTI) pamoja na wadau wa sekta ya biashara Tanzania, ikiwa sehemu ya kampeni endelevu ya kuhamasisha matumizi ya nembo ya Made in Tanzania. 
Katika mkutano huo “Mamlaka ya TanTrade imefungua macho ya wazalishaji kwa kuonyesha kuwa muda umefika wa kuunganisha nguvu  kati yao na Serikali katika kuongeza juhudi za kufikia masoko ya ndani na ya nje ya nchi. Kupitia matumizi ya nembo ya Made in Tanzania, wazalishaji wanapata fursa ya kutambulika rasmi na serikali, uwezo wao kuthaminiwa, na bidhaa zao kuunganishwa na masoko ya ndani na nje ya nchi. Nembo hii ni chombo cha ushindani na heshima ya kitaifa, hususan katika zama mpya za biashara huria barani Afrika. TanTrade inatoa wito kwa wazalishaji wote kujisajili sasa ili kunufaika na fursa hizi, kuongeza thamani ya bidhaa zao, na kujenga imani ya watumiaji kwa bidhaa za Tanzania.”
Wanachama wa CTI na wadau wengine walioshiriki walipata nafasi ya kutoa maoni na uzoefu wao, wakieleza fursa zinazopatikana kupitia sekta ya viwanda sambamba na changamoto za gharama za uzalishaji na upatikanaji wa masoko. Kwa pamoja, walikubaliana kuimarisha kampeni ya Made in Tanzania ili kuongeza ajira, kukuza uchumi wa taifa, na kujenga imani ya watumiaji kwa bidhaa za ndani.