KATIBU MKUU WA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA ZANZIBAR ATEMBELEA SABASABA 2025.
- July 5, 2025

5 JULAI, 2025.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Maendeleo ya Biashara Zanzibar Bi. Fatma Mabrook ametembelea Maonesho ya SabaSaba ikiwa siku ya nane toka maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yaanze. Bi. Fatma amewataka wafanyabiashara mbalimbali kutoka Zanzibar wanaojihusisha na biashara ya Mwani, Viungo na Utalii kuendelea kuchukua fursa kubwa kama hii kwa maendeleo endelevu ya uchumi wa Buluu. Maonesho ya Sabasaba 2025 yamebeba kauli mbiu inayosema "Maonesho ya Biashara ya Kimataifa "SABASABA fahari ya Tanzania". Maonesho ya Sabasaba yanafanyika katika kiwanja cha Mwl. Julius Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam. (Sabasaba Grounds)