Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

KATIBU MKUU WA VIWANDA NA BIASHARA AKABIDHI NYARAKA ZA OFISI KWA MWENYEKITI WA BODI MPYA YA TANTRADE.

  • August 28, 2025

27 Agosti, 2025.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Tanzania Dkt. Hashil T. Abdallah amekabidhi nyaraka za ofisi kwa Mwenyekiti wa Bodi mpya ya wakurugenzi ya TanTrade, Profesa Ulingeta O.L Mbamba  leo katika ofisi za TanTrade jijini Dar es salaam.

Akikabidhi Nyaraka hizo Dkt. Hashil ameiomba bodi hiyo kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha miradi mbalimbali ya Taasisi inafanya vizuri hususani  Mradi wa Uendelezaji wa Uwanja wa Maonesho wa Mwl. J.K Nyerere pamoja na kuhakikisha shughuli zote za kibiashara zinazokuwa chini ya Mamlaka zinakwenda vizuri kama inavyotakiwa.

Kadhalika alisisitiza, "Bodi na majukumu yake yapo kwa mujibu  wa sheria , hivyo wasimamie hayo". Vilevile, alimsisitiza Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Dkt. Latifa M. Khamis pamoja na Menejimenti yake, kusimamia na kutekeleza majukumu ya Taasisi  kwa mujibu wa Sheria.