Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

RAIS WA MSUMBIJI ATEMBELEA BANDA LA TANTRADE LILILOPO NDANI YA BANDA LA TANZANIA KWENYE MAONESHO YA 60 FACIM 2025 MAPUTO MSUMBIJI

  • September 1, 2025

Rais wa Msumbiji, Mhe. Daniel Chapo, ametembelea Banda la TanTrade katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa 60 FACIM, akiambatana na mwenyeji wake Mhe. Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji Hamad Khamis Hamad. Kwa mujibu wa Afisa wa TanTrade Bw. Josephat  Bwathondi, ameeleza kuwa Tanzania kupitia TanTrade inaendelea kutangaza bidhaa na huduma mbalimbali ikiwemo Korosho, Kahawa, Asali ya Moringa, viungo kutoka Zanzibar, Michoro ya sanaa ya Tingatinga, Mavazi, na Chai.
Mhe Rais, ameipongeza TanTrade kwa jitihada wanazofanya za kutangaza bidhaa za Tanzania katika Maonesho yanayoendelea Nchini huko. Maonesho hayo, yanayotaraji kutamatika Agosti 31, 2025, yatafungua fursa ya Masoko hususan Nchini Msumbiji.