Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

NEMBO YA TAIFA "MADE IN TANZANIA" MKOMBOZI WA BIDHAA NA HUDUMA ZA TANZANIA.

  • July 8, 2025

8 JULAI, 2025.


Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Tanzania Mhe. Exahud Kigahe (Mb) ameipongeza Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kwa kufanikisha nembo/ rajamu ya Taifa "Made in Tanzania ". Naibu Waziri ameainisha kuwa kupitia nembo hiyo Tanzania inakwenda kupata Mapinduzi ya mafanikio ya Biashara na Uchumi kwa wazalishaji wa bidhaa na huduma wa hapa nchini Tanzania.
 Aidha Naibu Waziri ametoa rai kwa Watanzania kutumia fursa ya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa katika kujitangaza, kuongeza masoko, na kushindani katika masoko ya Kimataifa ameainisha hayo katika Kongamano la Uhamasishaji wa matumizi ya Nembo ya Taifa ya "Made in Tanzania". Lilifanyika siku ya Kumi na Moja ya  Maonesho ya Sabasaba 2025.