MAONESHO YA 49 YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA DAR ES SALAAM, SABASABA 2025 YABORESHWA KWA VIWANGO VYA KIMATAIFA.
- June 28, 2025
28 JUNI 2025.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania TanTrade Bi. Latifa M. Khamis amezungumza na Waandishi wa Habari siku ya kwanza ya Maonesho na kuainisha maboresho mbalimbali katika Maonesho ya Sabasaba 2025 msimu wa 49. Maboresho hayo yamefanyika kwenye mifumo mbalimbali ya kuchukua nafasi (mabanda) kukata tiketi za viingilio pamoja na malipo ya maegesho ya magari lakini pia TanTrade kwa kushirikiana na Posta wamewaletea Watanzania watakao tembelea Maonesho huduma ya Usafiri wa ndani ya Viwanja vya Maonesho kwa gharama nafuu ya kusafirisha mizigo yao kutoka Sabasaba kwenda majumbani kwao, ameainisha hayo katika mkutano wake na Waandishi wa Habari uliofanyika katika Ofisi za TanTrade zilizopo katika kiwanja cha Mwl. Julius Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.