TFF NA TANTRADE ZAJIPANGA KUWAPA BURUDANI WATEMBELEAJI WA MAONESHO YA 49 SABASABA 2025
- June 17, 2025
17 JUNI, 2025
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania TanTrade Bi. Latifa M. Khamis amezungumza na Ndugu Adam Ng'amba ambae amemuwakilisha rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kuangazia maandalizi ya ushiriki yanayofanywa na Shirikisho hilo katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, Sabasaba 2025.
TFF imejipanga kushiriki kikamilifu Maonesho haya ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yenye fursa mbalimbali. TFF itawaleta wachezaji nguli wa mpira wa miguu kutoka vilabu mashuhuri nchini jambo litakalowapatia fursa watembeleaji kutoka ndani na nje ya Tanzania kuwaona wachezaji hao, fursa ya kuona na kununua jezi za timu ya taifa sambamba na kujifunza maswala mbalimbali ya mpira wa miguu kwa lengo na kukuza na kuendeleza mchezo huo wenye mamilioni wa wafuatiliaji, leo katika Ofisi za TanTrade zilizopo katika kiwanja cha Mwl. Julius Nyerere barabara ya kilwa