Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANZANIA INVEST NA TANTRADE KUPEPERUSHA BENDERA MAONESHO YA SABASABA, NEMBO YA TAIFA NA MRADI WA KUENDELEZA UWANJA WA MWL. JULIUS NYERERE (SABASABA GROUNDS)

  • June 24, 2025

23 JUNI, 2025.

Kituo cha Habari cha Tanzania Invest kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) wanuia kuunganisha nguvu katika kutangaza Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam Sabasaba, Nembo ya taifa "Made in Tanzania" sambamba na kunadi Mradi wa kuendeleza Uwanja wa Mwl. Julius Nyerere Sabasaba (Grounds), mazungumzo haya yamefanyika leo katika kikao kilichoongozwa na Bi Latifa M Khamis Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania TanTrade  na Mwakilishi wa Tanzania Invest Bwa. Eric Tirabasi katika Ofisi za TanTrade zilizopo katika kiwanja cha Mwl. Julius Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.