Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE YASHIRIKI KONGAMANO LA FEDHA, KAZI NA KUJITEGEMEA KWA VIJANA NA WANAWAKE KWENYE MAONESHO YA KIMATAIFA YA KILIMO NANENANE 2025.

  • August 8, 2025

7 AGOSTI, 2025.



Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imeshiriki kikamilifu Kongamano la fedha Kazi na kujitegemea kwa Vijana na Wanawake kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane 2025. Kongamano hilo limeangazia namna ya vijana  kuwa na nidhamu ya fedha na mbinu mbalimbali za kufanikiwa kwenye biashara. 
Aidha TanTrade kama Taasisi yenye jukumu la kuendeleza na kukuza biashara nchini ipo Kwa lengo la kujulisha Umma mifumo ya taarifa za Biashara na Masoko ya ndani na Kimataifa, Kujenga uwezo wa sekta ya Biashara, Kufanya tafiti za kimasoko nk. Kongamano hilo linafanyika katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane katika Kiwanja cha Nzuguni, Jijini Dodoma.