TANTRADE YAENDELEA KUTOA MAFUNZO KWA WAFANYABIASHARA MATUMIZI YA TRADE PORTAL
- May 20, 2025
Moshi – Kilimanjaro.
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imetoa mafunzo ya matumizi ya mfumo wa uingizaji na usafirishaji wa bidhaa nje ya nchi Trade Portal katika semina iliyoandaliwa kwa kushirikiana na Baraza la Biashara la Afrika Mashariki ambapo jumla ya wafanyabiashara 45 kutoka mkoa wa Kilimanjaro walihudhuria katika semina hiyo iliyofanyika katika hotel ya Selinaro Moshi – Kilimanjaro.
Aidha Mafunzo hayo kwa wafanyabiashara hao yalilenga kuwajengea uwezo wa namna ya kutumia mfumo wa Trade portal kufahamu taratibu za usafirishaji, kuagiza au kupitisha mazao na bidhaa nje ya nchi. Pia kuwaonesha namna gani mfumo unatoa wasaa wa kupata usaidizi katika kutatua changamoto wanazokutana nazo mipakani ( exit point) na kuitaarifu TanTrade na hivyo kuwasaidia kuzitatua.