Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE NA POSTA ZAUNGANA KUTOA HUDUMA ZA USAFIRI WA WATU NA MIZIGO KWENYE MAONESHO YA SABASABA 2025.

  • June 18, 2025

3 Juni 2025
Dar es Salaam

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kwa kushirikiana na Shirika la Usafirishaji Posta wameungana ili kutoa huduma  ya usafirishaji watu na bidhaa mbalimbali katika kipindi cha Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) 2025 ili kuepusha usumbufu wa usafirishaji kwa washiriki na watembeleaji wa maonesho ya Sabasaba.

Aidha Shirika la Posta litakuwa huduma ya SwifPack ambayo ni huduma ya magari maalum yatakayobeba watu mbalimbali ndani  ya maonesho kwa gharama nafuu sambamba na mizigo yao, hatua hii imelenga zaidi kuboresha huduma za maonesho kwa umma wa wafananya biashara, Maonesho haya ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam Sabasaba 2025 yanaratibiwa na TanTrade na yataanza rasmi tarehe 28 Juni 2025 hadi tarehe 13 Julai 2025.

Tukio hili la uzinduzi limetokea leo Makao Makuu ya Posta jijini Dar es salaam.