Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

KARIBUNI MUWEKEZE KWENYE MRADI WA KUBORESHA UWANJA WA MAONESHO WA MWL. JULIUS NYERERE (SABASABA GROUNDS)

  • September 9, 2025

8 SEPTEMBA, 2025.


Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania TanTrade imeshiriki mkutano wa Kibiashara baina ya Tanzania na Omani ulioangazia masuala kadha wa kadha ya biashara na uwekezajı na fursa za masoko zilizopo baina ya mataifa hayo mawili. Kupitia mkutano huo,  TanTrade iliwasilisha hali ya biashara kati ya Tanzania na Oman na kuwakaribisha wawekezaji kwenye mradi wake makini wa kuendeleza uwanja wa Maonesho wa Mwl. J.K Nyerere (Sabasaba Grounds) ili kuwa wa viwango vya Kimataifa na kuvutia waoneshaji na watembeleaji wengi zaidi. Uwanja huu, hutumika katika uratibu wa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu (Sabasaba) ambayo hufanyika kila mwaka na kuwakutanisha wafanyabiashara kutoka Afrika na Mataifa mbalimbali ulimwenguni takribani 23. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam.