WAZIRI JAFO AWAKARIBISHA WATANZANIA KUTEMBELEA MAONESHO YA SABASABA 2025, MSIMU WA 49.
- July 2, 2025
2 JULAI, 2025.
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Selamani Jafo amewakaribisha Watanzania wote kutoka mikoa yote kuja Dar es Salaam na kutembelea Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam SABASABA 2025 kwa lengo la kutumia fursa mbalimbali zinazopatikana katika Maonesho ya Sabasaba 2025 kama vile huduma za kijamanii, burudani kutoka Kijiji cha Sanaa, punguzo la bei kwenye bidhaa mbalimbali. Ameainisha hayo wakati akitembelea Maonesho ya Sabasaba 2025 msimu wa 49 yanayoendelea katika kiwanja cha Mwl. Julius Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam. (Sabasaba Grounds).