Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

LONDON INSTITUTE OF SKILLS DEVELOPMENT AND OXFORD CLUB WAMTUNUKIA MKURUGENZI MKUU WA TANTRADE UDAKTARI WA HESHIMA WA WA BIASHARA NA UCHUMI

  • July 24, 2025

London
23 Julai, 2025

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Bi. Latifa M. Khamis ametunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Biashara na Uchumi kutokana na mchango wake mkubwa katika kukuza biashara na diplomasia ya uchumi kati ya Tanzania na nchi nyingine. 

Tuzo hiyo imetolewa na London Institute of Skills Development and Oxford Club kama uthibitisho wa juhudi, umahiri na mafanikio ya Dkt. Latifa katika kusimamia kwa ufanisi majukumu ya TanTrade, ambayo yamechochea maendeleo ya sekta ya biashara nchini na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa wa kiuchumi.