TUTUMIE MAONESHO YA SABASABA 2025 MSIMU WA 49 KUTANGAZA BIDHAA NA HUDUMA ZA TANZANIA
- June 29, 2025
29 JUNI 2025.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa ametoa rai kwa Watanzania kujitokeza na kutembelea Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam Sabasaba 2025, na kujipatia fursa ya kupata burudani kupitia Kijiji Cha Sanaa ambacho kimejipanga kuwaburudisha watembeleaji wa Maonesho hayo, pia kupata huduma za kijamanii kutoka taasisi binafsi na zauma. Kupitia Kijiji Cha sanaa kutakuwepo na timu mbalimbali za ligi kuu ambapo watembeleaji watapata fursa ya kuwaona wachezaji mbalimbali wa mpira wa miguu ameyasema hayo katika mkutano wake na waandishi wa Habari ulioratibiwa na Idara ya Habari Maelezo katika kiwanja cha Mwl. Julius Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam