Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

WAZIRI MSTAAFU WA FEDHA NA SPIKA MSTAAFU WA COMORO ATEMBELEA TANTRADE KUJADILI FURSA ZA BIASHARA

  • April 10, 2026


10 Aprili,2026

Waziri Mstaafu wa Fedha na Spika Mstaafu wa Comoro, Mheshimiwa Said A. Mchangama, ametembelea Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kwa lengo la kujadili na kuimarisha fursa za kibiashara kati ya Tanzania na Comoro.

Katika majadiliano hayo, takwimu za biashara zimeonesha kuwa katika kipindi cha miaka mitatu (2023–2025), Tanzania imeuza bidhaa zenye thamani ya dola za Marekani milioni 48.85 kwenda Comoro, huku Comoro ikiingiza bidhaa zenye thamani ya dola za Marekani milioni 0.014 pekee nchini Tanzania. Hali hii inaonesha wazi uwepo wa pengo kubwa la kibiashara pamoja na fursa pana kwa Tanzania kuongeza mauzo yake katika soko la Comoro.

Aidha, Waziri huyo mstaafu amesema kuwa kuna fursa kubwa ya kuuza bidhaa mbalimbali nchini Comoro. Baadhi ya bidhaa zenye uhitaji mkubwa ni pamoja na pamba, fanicha, vinywaji, bidhaa za plastiki, matunda na mboga mboga, mchele, mafuta ya kula, magodoro, maji ya kunywa, sabuni, saruji pamoja na nyama ya kuku.

Kadhalika, hii ni fursa kwa wafanyabiashara wa Kitanzania kutumia ipasavyo fursa hii kwa kuimarisha uzalishaji wa bidhaa zenye ubora na kuzipeleka katika soko la Comoro ili kukuza biashara na uchumi wa taifa.