PONGEZI TANTRADE KWA HATUA NJEMA ZA MAANDALIZI SABASABA 2025 MSIBU WA 49.
- June 24, 2025
23 JUNI 2025.
Mkuu wa Wiliya ya Temeke Mhe. Sixtus Mapunda ameipongeza TanTrade kwa kusimamia vyema maandalizi ya Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam Sabasaba 2025. Kupitia ziara yake ya kukagua uwanja wa Maonesho Mhe. Mapunda amewakaribisha Watanzania wote kuja kutembelea Maonesho ya Sabasaba yatakayoanza tarehe 28 Juni mpaka 13 Julai 2025.
Aidha ametoa rai kwa makampuni yote ya usafirishaji, na wamiliki wa malori kutokupaki magari hayo karibu na pembezoni mwa maeneo ya uwanja wa maonesho wa SABASABA, leo katika kiwanja cha Mwl. Julius Nyerere (Sabasaba Grounds) barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.