Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

MKUU WA WILAYA YA CHATO AVUTIWA NA MCHELE MWEUSI WENYE NEMBO YA MADE IN TANZANIA

  • September 29, 2026


29 Septemba 2026 Geita

Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhe. Louis Peter Bura, ameipongeza Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kwa kuwapa wazalishaji wa ndani nafasi ya kutangaza bidhaa zao na kuunganishwa na fursa za masoko ya ndani na nje ya nchi.

Mhe. Bura ametoa pongezi hizo alipotembelea banda la TanTrade katika Maonesho ya Tisa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika mkoani Geita. Akiwa bandani hapo, alivutiwa na mchele mweusi wa MOMO BLACK RICE, miongoni mwa bidhaa za wazalishaji wanaoshiriki kupitia TanTrade na zilizo na Nembo ya Taifa ya Made in Tanzania.

Aidha, amewapongeza wazalishaji wengine, akiwemo MIMII WINE, kwa kutumia maonesho hayo kutambulisha bidhaa zao kwa wananchi na wadau wa biashara. Amesema nembo ya Made in Tanzania inasaidia kuongeza utambulisho wa bidhaa zinazozalishwa nchini na kuwapa wazalishaji nafasi ya kujenga uaminifu katika masoko mbalimbali.

Mhe. Bura amehimiza TanTrade kuendelea kushirikiana na wazalishaji pamoja na taasisi zinazotoa huduma za biashara ili kuimarisha uwezo wa bidhaa za Kitanzania kushindana na kufikia masoko mapya.