WAFANYABIASHARA WAKUBWA TOKA KOREA WAJA NA FURSA ZA BIASHARA KWA BIDHAA ZA MADE IN TANZANIA
- November 26, 2025
26 Novemba, 2025.
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imeratibu na kushiriki kongamano la Biashara baina ya Makampuni ya Tanzania na Waagizaji Bidhaa kutoka Korea- KOIMA lililoangazia kuimarisha ushirikiano yakinifu wa biashara kwa kuzingatia Maendeleo ya Biashara na Uchumi baina ya nchi hizo mbili, Dkt. Latifa M. Khamis Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade akizungumza kwa upande wa Tanzania ameainisha mambo mbalimbali ikiwemo, kuhamsisha wafanyabiashara wa Tanzania kuchukua fursa za Biashara zinazohitajika Korea Kwani Makampuni 15 yaliyokuja ni makubwa nchini humo na hununua bidhaa kwa zenye ubora na kiwango cha juu zenye thamani ya zaidi ya USD milioni 700 kwa mwaka, Hivyo ametoa Rai kwa wazalishaji wa Tanzania kuhakikisha wanasajili bidhaa zao na alama rasmi ya Made in Tanzania ili kuweka urahisi kufanya biashara kwenye masoko ya kimataifa