MWALIKO WA UFADHILI WA MAONESHO YA 44 YA DITF

Imewekwa: Mar 28, 2020


Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) inapenda kuwatangazia Washiriki wa Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam(44th DITF, 2020),Taasisi za Umma na Binafsi, Makampuni, Wafanyabiashara na Umma kwa ujumla kuhusu fursa za udhamini wa Maonesho hayo katika vifurushi vifuatavyo:-

1. Mdhamini Mkuu wa Mawasiliano

2. Mdhamini wa Sherehe za Ufunguzi na Ufungaji

3. Mdhamini Mkuu wa Huduma za Kibenki

4. Mbia Mkuu wa Matangazo

5. Mbia wa Bima

6. Mbia wa Huduma za Usafiri

7. Mbia wa Ujenzi

8. Mdhamini wa Matangazo ya Umma ndani ya Uwanja

9. Mdhamini wa Vinywaji na Vyakula

10. Mdhamini wa Huduma za Mtandao

11. Mdhamini wa Mikutano ya Wafanyabiashara ya Ana kwa Ana(B2B Meetings)

12. Mdhamini wa Siku Maalum

13. Mdhamini wa Burudani

14. Mdhamini wa Michezo ya Watoto

15. Mdhamini wa Taa za Mitaani

16. Mdhamini wa Bustani

Kwa maelezo zaidi kuhusu vifurushi hivi, utaratibu na udhamini kwa ujumla, tafadhali wasiliana nasi kupita barua pepe ifuatayo info@tantrade.go.tz, au piga simu ya mkononi Na. 0767 616 617 au fika Ofisini kwetu Uwanja wa Maonesho wa Mwl. J.K. Nyerere, Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 17 April, 2020.

Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu,
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade),
P.O. Box 5402,
DAR ES SALAAAM.
Simu ya Mezani: +255 22 2850 153
Tovuti: www.tantrade.go.tz