Habari

Imewekwa: 26/09/2018

TADB YAUNGANA NA TANTRADE KULIVAA SOKO LA CHINA

TADB YAUNGANA NA TANTRADE KULIVAA SOKO LA CHINA

Benki ya Kilimo ya Tanzania(TADB) kuungana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania(TanTrade) katika kuwawezesha wafanyabiashara Nchini kuingia katika soko la China,ikiwa ni pamoja na kuwawezesha wafanyabishara wa mazao ya kilimo kupata mitaji itakayowawezesha kuzalisha bidhaa zitakazotosheleza mahitaji ya soko la China.
Akizungumza katika kikao kilicholenga kuwawezesha wakulima kuingia katika soko la China Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Kilimo(TADB) Bw.Japhet Justine amesema TADB itawakopesha wakulima kwa kuwa kunauhakika wa soko.
Justine amesema uwepo wa soko la China kutaondoa changamoto ya wakulima kushindwa kufanya marejesho ya mkopo kwa kisingizio cha kutokuuza mazao.
Ameongeza kuwa TADB ni benki iliolenga kumuendeleza mkulima ikiwa ni pamoja na kuunga mkono jitihada za kumuwezesha kupata soko kwa bei nzuri. "...Sisi tunawahudumia wakulima na kutoa mitaji lakini TanTrade wametafuta soko”
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bw.Edwin Rutageruka amesema TanTrade ilipeleka sampuli mbalimbali za mazao na bidhaa za Tanzania katika Maonesho ya Kimataifa ya 15 ya CAEXPO 2018 Nanning China,ambapo bidhaa zilizo sindikwa zilipata soko kubwa ikiwa ni pamoja na mbaazi,tangawizi,choroko,asali na dengu.
Katika Maonesho hayo kwa 2018 Tanzania ilikuwa mgeni mashuhuri ambapo TanTrade iliratibu Maonesho hayo na Taasisi za Serikali bara na Zanzibar,jumuiya ya wafanyabiashara na wajasiliamali wapatao 50 walishiriki maonesho hayo.
Katika Picha:Kaimu Mkurugenzi TADB Bw.Japhet Justine(kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bw.Edwin Rutageruka
Kitengo Cha Mawasiliano