Habari

Imewekwa: 24/02/2019

SOKO LA BIDHAA ZA TANZANIA NCHINI UKRAINE LAWEKWA WAZI

 SOKO LA BIDHAA ZA TANZANIA NCHINI UKRAINE LAWEKWA WAZI

Ukraine imetenga kanda mbalimbali ulimwenguni ambazo zinatija kwa bidhaa zinazotoka Ukraine pamoja na kutafuta bidhaa zitakazo ingizwa kwenye soko la Ukraine kutoka katika nchi hizo,ambapo Tanzania ni moja kati ya nchi zinazopewa kipaumbele.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Ukuzaji Masoko Bi Rita Polishchuk kutoka Taasisi inayosimamia Biashara ya Kimataifa nchini Ukraine wakati wa mkutano maalum wa kujadili fursa za kibiashara baina ya Tanzania na Ukraine ulioandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania(TanTrade) kwa kushirikiana na Taasisi inayosimamia Biashara ya Kimataifa ya Ukraine(Trade with Ukraine) uliofanyika Februari 19,2019 katika Uwanja wa Maonesho wa Mwl J.K.Nyerere,Barabara ya Kilwa Dar es salaam.

Bi.Polishchuk alisema, Ukraine imeadhimia kufungua kituo cha kibiashara kati ya Tanzania na Ukraine kitakachosaidia wafanyabiashara wa Tanzania kupeleka bidhaa na huduma nchini Ukraine.Kituo hicho kitaisaidia Ukraine kuingiza bidhaa mbalimbali Tanzania hususan mashine, pia kitawasaidia Watanzania kuepuka vikwazo vya biashara vya kiushuru na visivyo vya kiushuru.

Amesema bidhaa zinazoitajika kutoka Tanzania ni mbogamboga,matunda,viungo vya chakula na kusisitiza kuwa bidhaa kama Kahawa,Chai na Kokoa zinahitajika kwa kiasi kikubwa,ambapo katika mkutano huo alieleza vigezo vinavyohitajika kuingiza bidhaa hizo Ukraine.

Nae Kaimu Meneja Utafiti na mipango TanTrade Bw.John Fwalo amesema TanTrade imeweza kuwaalika wadau mbalimbali ili kuwawezesha Watanzania kwenda kuuza kwenye soko la Ukraine.

“Tunasajili wadau wote walioweza kufika ili kuweza kutambua ni aina gani ya wadau wamekuja kushiriki kwenye mkutano huu, tutawafuatilia kwa ukaribu hatua walizofikia katika kufanya biashara na nchi ya Ukraine pia tutaweza kubaina kwa ukaribu kama kutakuwa na changamoto zitakazowakabili.Tutaendelea kuwajengea uwezo ili waweze kufanikiwa kwa kuwa na masoko endelevu’’ Alisema Fwalo

Mwenyekiti wa Chama Cha Wasindikaji Vyakula nchini(TAFOPA) Bi Suzy Leizer ambaye ameshiriki mkutano huu amesema wameambiwa kuwa bidhaa ya Chia Seed inahitajika kwa kiasi kikubwa,hivyo ameishukuru TanTrade kwa kuwaunganisha na soko la Ukraine.

Amewaomba wakulima kuungana ili kuweza kumudu mahitaji ya soko la nje ambalo linamahitaji makubwa ya bidhaa na ni vigumu kwa mtu mmoja mmoja kulimudu.

Silivester Kapya mkulima wa Kijiji cha Kipanga Wilaya ya Sikonge,Mkoani Tabora ameeleza kuwa amefurahi kukutana na mtalamu kutoka Ukraine ambae amehaidi kumuunganisha na Wafanyabiashara wenye mashine za kisasa za kusagia Karanga kutoka Ukrainea ambao watamsaidia kuwekeza zaidi katika mitambo ya kuchakata.