Habari

Imewekwa: 13/06/2018

MAHUSIANO YA KIBIASHARA KATI YA KOREA-KUSINI NA TANZANIA KUIMARIKA ZAIDI

MAHUSIANO YA KIBIASHARA KATI YA KOREA-KUSINI NA TANZANIA KUIMARIKA ZAIDI

Be the first to like tantrade_official Instagram page

Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Biashara cha Korea- Kusini (KOTRA) Lee,Hong-Kyun ametembelea Ofisi za Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) na kufanya Mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu Bw.Edwin Rutageruka.

Mazungumzo hayo yamelenga Kuimarisha Mahusiano ya Biashara Kati ya Tanzania na Korea Kusini ,ikiwa ni pamoja na kuhamasisha makampuni kushiriki Maonesho na Misafara ya Biashara ili kuweza kutambua fulsa zilizopo baina ya nchi hizi mbili.

Lee,Hong-Kyun aliongozana Afisa wa KOTRA anayesimamia masuala ya Utafiti na Masoko Bi.Catherine James walipata fulsa ya kujionea maandalizi ya Maonesho ya Kimataifa ya Dar es Salaam(SabaSaba) na kuongozwa na Mkuu wa Itifaki kutoka TanTrade Bi.Twilumba Mlelwa.