Habari

Imewekwa: 04/10/2018

KABAKA KUTEMBELEA SOKO LA SABASABA

KABAKA KUTEMBELEA SOKO LA SABASABA

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Taifa(UWT) Mh.Gaudentia Kabaka ameahidi kutembelea Soko la SabaSaba ili kujionea ushiriki wa Wanawake Wajasiliamali katika soko hilo.
Kabaka ametoa ahadi hiyo leo mara alipotembelea TanTrade Dar es Salaam,ambapo alipewa maelezo juu ya uwepo wa soko hilo linalofanyika kila Jumamosi na Jumapili katika uwanja wa Mwl.J.K Nyerere(Barabara ya Kilwa Dar es Salaam).
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bw.Edwin Rutageruka amewakaribisha pia Wanawake Wenye Viwanda Vidogo,Vya kati na Vikubwa kujitokeza kushiriki Maonesho ya Viwanda ya Tanzania yanayotarijia kuanzia tarehe 5 hadi 9 Desemba,2018 katika uwanja Mwl.J.K Nyerere(Barabara ya Kilwa Dar es Salaam).