Habari

Imewekwa: 08/09/2018

DARASA LA WASIONA TANTRADE KUPATIWA VYEREHANI

DARASA LA WASIONA TANTRADE KUPATIWA VYEREHANI

Naibu Waziri Sera, Bunge,Ajira,Vijana na Walemavu Stella Ikupa ameahidi kutoa vyerehani vitano kwa Kiwanda Darasa Cha Walemavu Wasiona kinachosimamiwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania(TanTrade).
Akiwa katika Darasa hilo Mh. Waziri alivutiwa na jitihada zinazofanywa na Walemavu Wasiona katika kujikwamua kiuchumi na kujitegemea katika kuendesha maisha yao.
Awali akiwa katika kongamano la Wajasiliamali Walemavu lilofanyika katika ukumbi wa SabaSaba uliopo kwenye Uwanja wa Mwl.J.K Nyerere Mh.Naibu Waziri alieleza kuwa nia yake ni kuhakikisha hakuna mlemavu ambaye atakuwa ombaomba. "kama kutakua na ombaomba basi asiwe mlemavu"
Katika Picha ni Mh. Naibu Waziri Stella Ikupa(Katikati) na Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bw. Edwin Rutageruka(kushoto) wakimsikiliza Mkufunzi wa Darasa la Wasiona Dkt.Abdalah Nyangalilo akiwaonesha namna mtu asieona anavyoweza kutunga uzi katika cherehani.